Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, ikinukuu kutoka katika tovuti ya habari ya "Akhbar Bahrain", Sheikh "Issa Ahmad Q'asim", mmoja wa maulamaa wa Bahrain, katika tamko lake alimtaja Ayatollah Khamenei Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, kuwa ni alama kubwa ya Qur’ani na uongozi wa nadra katika zama hizi, na akaongeza kuwa nafasi hiyo kuu ya tablighi na uwezo wa kuwainua Waislamu inaonesha uaminifu wake wa dhati kwa Qur’ani na utukufu wa hali ya juu wa mheshimiwa huyo, ambao umetokana na ikhlasi yake kwa nguvu ya Uislamu.
Kiongozi huyo wa Waislamu wa Kishia nchini Bahrain aliongeza kuwa: Kuwepo mazingira yoyote ya maneno ya matusi au vitisho dhidi ya mtukufu huyu (Ayatollah Khamenei) ni matusi kwa Umma mzima wa Kiislamu na vitu vyake vitakatifu pamoja na nafasi ya fiqhi takatifu.
Akiashiria kwamba matusi na vitisho vya Trump dhidi ya nafasi hiyo tukufu ni ujinga, upumbavu na vinaonesha ukosefu wa umakini katika tathmini ya mambo na matokeo yake, aliongeza kuwa: Hili ni tusi na tishio kwa Umma mzima wa Kiislamu na kwa vitu vyote vitukufu vyetu, jambo ambalo linaweka jukumu zito juu ya mabega ya Umma mtukufu wa Kiislamu.
Maoni yako